March 29, 2021


 KOCHA wa Klabu ya AS Vita, Flolent Ibenge leo ana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Gambia kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Afcon itakayochezwa nchini Cameroon.

Mbali na kuwa kocha wa Klabu ya AS Vita, Ibenge pia ni kocha wa timu ya taifa ya DR Congo iliyo kundi D na ipo nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 6.

Imekwama kukata tiketi ya kushiriki Afcon kwa sababu pointi zake ni chache kuliko wapinzani wao Gambia ambao wapo nafasi ya pili na wamekusanya pointi 10.

Kinara wa kundi D ni Gabon naye pia ana pointi 10 wakitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa na wale walio nafasi ya pili na nafasi ya nne ipo na Angola yenye pointi moja.

Gabon imefunga mabao 8 na kufungwa mabao manne huku Gambia wamekiwa wamefunga mabao 9 na kufungwa mabao 6.

Ibenge akimalizana na Gambia leo ana kazi ya kukinoa kikosi chake cha AS Vita kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba ambao unatarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza walipokutana Ibenge alishuhudia Simba ikisepa na pointi tatu kwa bao la Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba ratiba kwake si rafiki ila atapambana kupata pointi tatu, Uwanja wa Mkapa.

"Kwa kweli kazi ni kubwa na ratiba pia haijawa rafiki kwangu kwa kuwa haya mashindano ya Afcon yanatufanya tunakuwa bize muda mwingi na ukizingatia pia ninaifundisha AS Vita.

"Muda unakuwa ni mchache lakini haina maana kwamba tutashindwa hapana tupo imara na tutafanya vizuri," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic