March 29, 2021


 NYASHA Charandura Kocha wa Viungo wa Klabu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu,George Lwandamina kwa sasa yupo zake nchini Zimbabwe.


Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa Nyasha yupo nchini Zimbabwe akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya nchi hiyo 'Warriors'.


Charandura aliyetua nchini kushika majukumu hayo mwishoni mwa mwaka jana, ndiye mtaalamu wa eneo hilo katika timu ya Taifa ya Zimbabwe.

Zimbabwe itashuka dimbani leo Jumatatu kuvaana na Zambia katika mchezo muhimu wa mwisho wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic