BONIPHACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer) amesema kuwa hajaridhishwa na ushindi wa mabao 8-3 walioupata dhidi ya Burundi.
Mchezo huo ambao uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa jana, Machi 30 ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon uliochezwa kwenye fukwe za Coco Beach, Dar.
Pawasa amesema kuwa kwa namna ambavyo walijiandaa aliamini kwamba wangepata ushindi mkubwa zaidi ya huo ili kuongeza hali ya kujiamini kwa vijana wake.
"Tulifanya maandalizi makubwa na mazuri jambo ambalo lilitupa matumaini kwamba tungepata ushindi mkubwa zaidi ya huu ambao tumeupata.
"Kwa kuwa kuna makosa ambayo tumeyaona tutayafanyia kazi ili wakati ujao tuweze kupata matokeo mazuri zaidi ya hapa.
"Ninawapongeza vijana kwa kazi ambayo wameifanya pamoja na sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakitupa nguvu sisi kufanya vizuri,".
Mchezo mwingine wa marudio dhidi ya Burundi unatarajiwa kuchezwa Aprili 3,2021
0 COMMENTS:
Post a Comment