MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kitu ambacho anakipenda kukifanya akiwa uwanjani ni kufunga mabao kwa ajili ya timu yake.
Nyota huyo raia wa Ghana ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi aliyechukua mikoba ya Cedric Kaze aliyefutwa kazi Machi 7.
Aliibuka Yanga akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda na kusaini dili la miaka miwili kuwatumikia Wanajangwani.
Yanga ikiwa imetupia jumla ya mabao 36 kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 23 amehusika katika mabao matano ambapo amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.
Sarpong amesema:-"Nikiwa uwanjani ninapenda kufunga na kuipa ushindi timu yangu hakuna jambo jingine ambalo huwa ninapenda. Ikitokea nikashindwa basi nitatengeneza nafasi kwa mwenzangu.
"Ukweli ni kwamba mashabiki wanapenda kuona timu ikishinda hilo ninalijua hata mwalimu pia amekuwa akituambia suala hilo, imani yangu nitafanya hivyo katika mechi zetu zijazo," .
Sarpong katika mabao hayo manne bao moja alifunga kwa mkwaju wa penalti ambapo ilikuwa Uwanja wa Mkapa na alimtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.
0 COMMENTS:
Post a Comment