March 20, 2021


NYOTA wawili wa klabu ya Simba, Luis Miquissone na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’, wametajwa katika kikosi bora cha wiki cha michuano ya klabu bingwa Afrika ambacho kina wachezaji 16 kutoka klabu sita.

Jumanne wiki hii Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudani ambapo, Luis na Zimbwe walihusika kwa kiasi kikubwa katika ushindi huo.

Luis alifunga bao moja na kuasisti bao la Chris Mugalu huku Zimbwe yeye akifanikiwa kufunga bao moja.

Ushindi huo umeifanya Simba sasa kufikisha pointi 10 na kuongoza msimamo wa kundi A la michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Simba inahitaji pointi moja kwa sasa ili iweze kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kundi A limekuwa na ushindani mkubwa ambapo timu inayomfuata Simba ni Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.


1 COMMENTS:

  1. Sasa hadithi zote Africa na nje ya Africa ni Mnyama tu na kutajea Konde Boy na Zimmbwe na wala si wengine au timu nyengine HAHAAA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic