SHABAN Kazumba, kocha msaidizi wa Tanzania Prisons amesema kuwa wapinzani wake ambao watakutana nao uwanjani ni lazima wajipange kukutana na pira gwaride kwa kuwa huo ni mwendo wao kwa sasa.
Prisons
inashikilia rekodi ya kuwapa tabu vigogo wa Bongo, Yanga na Simba ambapo timu
hizo mbili zote hazijaambulia ushindi kwenye mechi mbili ambazo walikutana nao.
Simba
zama za Sven Vandenbroeck ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na ule wa pili zama za
Didier Gomes, ngoma ilikuwa 1-1 na kwa Yanga mechi zote mbili ngoma ilikuwa
1-1.
Kazumba amesema:”Sisi tunacheza kwa afya na mwendo wetu
ni pira gwaride, tukikutana na timu za jeshi hapo kidogo huwa tunakwenda nao sawa
kwa kuwa nao wanacheza aina ya mpira wetu ila wapinzani wetu lazima wajipange
kwa pira gwaride,”.
Prisons
ipo nafasi ya 8 ina 31 baaada ya kucheza jumla ya mechi 23.







Mpira wa viatu balaa
ReplyDeleteKocha mzima unajobunia mpira wa kihuni?
ReplyDeleteIfike mahali timu za majeshi zizuiliwe kushiriki ligi zote zinazosimamiwa na tff. Mpira ni burudani na sio vita. Yaani watu wazima na akili zao wanajivunia vita kwenye mpira? Shame on them
ReplyDelete