March 29, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa haujapokea ofa yoyote kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini juu ya kiungo wao mkabaji Mkongomani Mukoko Tonombe kuhitajika huko.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu zizagae tetesi za kiungo huyo aliyejiunga na Yanga katika msimu huu akitokea AS Vita ya Kinshasa, Congo kuwaniwa na Chiefs.

 

Hivi karibuni Skauti Mkuu wa Klabu ya Kaizer Chiefs, Walter Steenbok alitua Bongo na kwenda kutembelea ofisi za klabu hiyo na kikubwa kujionea jinsi inavyojiendesha baada ya kupata taarifa za Tonombe na Tuisila Kisinda kujiunga na klabu hiyo msimu huu.


 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya Chiefs na Yanga kuhusiana na Tonombe.


Bumbuli alisema kuwa kilichopo hivi sasa ni mahusiano mazuri waliyoyajenga hivi karibuni kati ya Yanga na Chiefs katika kupata maendeleo ya soka nchini.


Aliongeza kuwa kwa upande wao Yanga hawana tatizo, hivyo wapo tayari kupokea ofa ya mchezaji yeyote kutoka klabu yoyote itakayomhitaji Tonombe na msataa wao wengine.

 

“Hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati ya Yanga na Chiefs, zaidi nizikaribishe klabu ambazo zitawahitaji wachezaji wetu.


“Yanga ni kati ya timu ambazo zimefanya usajili mzuri wa wachezaji wengi walio bora, hilo lipo wazi kabisa na hiyo ndiyo sababu ya sisi kuongoza ligi,” alisema Bumbuli.


Chanzo: Championi 

2 COMMENTS:

  1. Jee munaikaribisha Simba vilevile?

    ReplyDelete
  2. Hamuongozi ligi kwa sababu ya ubora wenu tu, Bali mnaongoza kwa sababu kubwa kwamba mshindani wenu Mkuu Simba Sports Club ana vipoeo vingi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic