RAZAK Siwa raia wa Kenya ametambulishwa rasmi na Klabu ya Yanga kuwa Kocha wa Makipa ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.
Benchi la Klabu ya Yanga iliyokuwa inanolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze lilifutwa rasmi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.
Anakuja kuchukua mikoba ya Vladinir Niyonkuru ambaye alikuwa akiwanoa akina Metacha Mnata, Faroukh Shikalo na Ramadhan Kabwili.
Mchakato wakumsaka kocha mkuu kwa sasa ndani ya Klabu ya Yanga unaendelea ambapo jina la Sebastian Mingne raia wa Ufaransa limekuwa likitajwa kuibuka ndani ya Yanga.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.
Ana kazi ya kulinda uwezo wa makipa wake kwa kuwa wamekuwa wakifungwa mabao ya aina moja ikiwa ni pamoja na Shikalo aliyeruhusu mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza Yanga kupoteza mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani.
Mnata naye kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid alikubali kufungwa bao la usiku kwa kushindwa kwenda na kasi ya mpira uliopigwa na Pius Buswitwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment