NYOTA wa Yanga, Wazir Junior ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Mbao FC ambaye alisaini dili la miaka miwili kwa dau la milioni 30 ametumia dakika 278 kupachika bao moja la ushindi kwenye mechi zake zote za ushindani alizocheza.
Mbele ya KMC wakati Yanga ikishinda mabao 2-1, Uwanja wa CCM Kirumba zama za Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 aliyeyusha dakika 81 na alifunga bao lake la kwanza.
Mechi yake ya pili ilikuwa mbele ya Biashara United wakati Yanga ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Karume, alitumia dakika 60 wakati Yanga ikilazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina, Uwanja wa Gwambina Complex alitumia dakika 58.
Wakati Yanga ikichezeshwa pira gwaride Uwanja wa Nelson Mandela na ubao kusoma Tanzania Prisons 1-1 Yanga alitumia dakika 13. Uwanja wa Amaan kwenye Kombe la Mapinduzi alitumia dakika 57 wakati Yanga ikilazimisha sare ya bila kufungana na Jamhuri na mchezo wa fainali mbele ya Simba alitumia dakika 7 ubao ulisoma 0-0.
Mchezo wake wa mwisho mbele ya Polisi Tanzania alitumia dakika mbili, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga.
Hivi karibuni, Wazir aliliambia Championi Jumatatu kuwa ikiwa atapata nafasi ya kucheza mechi nyingi kikosi cha kwanza atafanya vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment