March 30, 2021

 


SERGIO Aguero, mshambuliaji wa Manchester City ataondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya mabosi wa timu yake kuweka wazi suala hilo kwa kuwa hatuongezewa mkataba.

Arguero alijiunga  na Manchester City akitokea Klabu ya Atletico Madrid kwa dau la pauni milioni 35 na anapewa nafasi ya kunyanyua taji la tano la Ligi Kuu England kwa kuwa amenyanyua mataji manne, FA taji moja, League Cup mara tano.

Nyota huyo mwenye miaka 32 amekuwa imara uwanjani akifunga jumla ya mabao 257 kwenye mashindano yote akiwa amecheza jumla ya mechi 384 anatajwa kuwekwa kwenye rada za Barcelona na Inter Milan ambao wanahitaji saini yake.

Mkataba wa raia huyo wa Argentina unameguka msimu huu. Mchezo wake wa kwanza ndani ya City ilikuwa dhidi ya Swansea, Uwanja wa Etihad wakati ubao ulisoma Manchester City 4-0 Swansea.

Anaingia kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote ndani ya City akifuatiwa na Eric Brook ambaye ana mabao 177, Tommy Johnson ana mabao 166. Anaongoza pia kwa kufunga hat trick akiwa nazo 12, Alan Shearer anazo 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic