March 2, 2021

 


FISTON Abdurazak nyota mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa anaamini atafunga mabao mengi ndani ya timu hiyo kwenye mashindano yote ambayo watashiriki.

Ikiwa imecheza mechi 21 ndani ya ligi ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 49 kibindoni msimu wa 2020/21.

Nafasi yake ni ya kwanza inafuatiwa kwa ukaribu na Simba yenye pointi 45 ipo nafasi ya pili na imecheza jumla ya mechi 19.

Machi 4 Yanga ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ya Juma Mgunda ambayo imeweka wazi kwamba itapambana kupata pointi tatu.

Nyota huyo ambaye alifunga bao pekee kwa mkwaju wa penalti wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold, Uwanja wa Uhuru mchezo wa Kombe la Shirikisho amesema kuwa bado kazi inaendelea.

"Kwa kuanza mbele ya Ken Gold ni mwanzo mzuri kwangu na kwa timu kiujumla hivyo bado kuna nafasi ya kufunga kwenye mechi nyingine zaidi.

"Najua kwamba mashabiki wanapenda kuona nikifunga nami nitapambana ili kuweza kufanya hivyo,".

2 COMMENTS:

  1. Hata Sarpong aliahidi sasa hv yuko kimya.... Acheni maneno mengi fanyeni kazi

    ReplyDelete
  2. Mpira Ni vitendo siyo porojo hata kwenye kanga yapo, magarasa Ni magarasa tu utayatambua kwa matendo na uwezo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic