March 28, 2021


 UNAAMBIWA huko kwenye kambi ya Yanga, Kaimu Kocha Mkuu wake, Juma Mwambusi, amejikuta akichanganyikiwa baada ya kupata taarifa za ghafla za kuugua kwa nyota wake tegemeo raia wa Burundi, Fiston Abdulazak na Michael Sarpong, raia wa Ghana.
 

Mwambusi aliingia kambini na kikosi hicho Jumatatu iliyopita baada ya kupisha shughuli fupi za kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Joseph Magufuli, zilizofanyika Machi, 20 na 21 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mwambusi ameweka wazi kwamba, takriban siku tatu zilizopita alijikuta akipata presha baada ya wachezaji wake wawili, Sarpong na Fiston kujikuta kwa pamoja wakishindwa kuendelea na program za mazoezi yake, kufuatia kukumbwa na homa nzito.

 

“Namshukuru Mungu kwa sasa wachezaji wangu takriban wote wako sawa na kwamba tunaendelea na program zetu za mazoezi asubuhi na jioni, ingawa kwa siku takriban nne nilipata hofu baada ya wachezaji wangu wawili ambaye ni Fiston na Sarpong kukumbwa na homa.

 

"Jambo ambalo ninamshukuru Mungu sasa wanaendelea vyema na bila shaka hadi kufikia Jumatatu ijayo watakuwa wamerejea mazoezini na kuendelea na program za pamoja hadi pale tutakapoanza ratiba za kujiandaa na michezo ya ligi kuu mara baada ya siku za maombolezo kuisha,” alisema Mwambusi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic