March 28, 2021

 

 

KOCHA wa viungo wa Yanga raia wa Ghana, Edem Mortotsi amesema kuwa kwa kipindi hiki cha mapumziko ya ligi amejikita zaidi kwenye kutengeneza utimamu wa mwili 'fitness' kwa wachezaji wake ambao walibaki kambini.

Akizungumzia hali za nyota wa kikosi hicho Mortotsi amesema wakati anakuja kwenye kikosi hicho alikuta baadhi ya wachezaji fitness yao ikiwa ya kawaida, hivyo jambo la kwanza alilofanya ni kuhakikisha wachezaji wote wanakuwa kwenye levo moja ya fitness jambo ambalo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Namshukuru Mungu kuwa kila kitu kinakwenda vizuri sana kwa upande wa wachezaji wangu, ukitazama utimamu wao wa mwili kwa sasa nitofauti na ilivyokuwa mwanzo.

"Kwa sasa wachezaji wote wameonyesha kuongezeka fitness jambo ambalo nilikuwa nalihitaji kuliona likifanikiwa wakati nilipofika kwenye timu hii,” alisema Edem.

Yanga ipo kwenye kambi yao Kigamboni Avic ikiendelea na maandalizi yao ya kumalizia michezo kadhaa ya ligi kuu chini ya kocha wa muda Juma Mwambusi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


1 COMMENTS:

  1. Tafuteni mechi za kutosha kujipima. Fitness na combination are equally crucial

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic