March 3, 2021


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kwamba unazihitaji pointi tatu za Dodoma Jiji, kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Mabatini leo Machi 3..

Ikiwa ipo nafasi ya 6 na pointi zake kibindoni ni 31 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 7 na pointi zake ni 29.


Timu zote mbili kwa msimu wa 2020/21 zimecheza jumla ya mechi 21.


Akizungumza na Saleh Jembe, Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wanahitaji pointi tatu ili kuweza kuyafikia malengo ambayo wamejiwekea.

“Tunahitaji pointi tatu ndani ya uwanja kwa kila mchezo kwetu ni lazima tufanye vizuri ili kuzidi kujikusanyia pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti.

"Wachezaji wapo tayari na wana morali kubwa, pia hakuna shida yoyote ndani ya timu sasa unadhani kwa nini tusifikirie pointi tatu ndani ya uwanja?

Mbwana Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa wapo tayari na wataingia ndani ya uwanja kwa tahadhari kusaka pointi tatu.

"Ushindani ni mkubwa na tunawaheshimu wapinzani wetu ila tupo tayari na tutaingia ndani ya uwanja kwa tahadhari tukihitaji pointi tatu,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic