March 28, 2021

 

MOTO anaoendelea kuuwasha kiungo, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ akiwa na kikosi cha Burundi, umeushitua Uongozi wa klabu ya Yanga, ambao sasa umepanga kuwarudisha haraka iwezekanavyo nyota wake walio kwenye vikosi vya timu za taifa mara tu watakapomaliza majukumu hayo.

Yanga ina nyota watatu wa kimataifa ambao wameitwa katika vikosi vya mataifa yao kwa ajili ya michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu AFCON.

Nyota hao ni Mukoko Tonombe (DR Congo), Haruna Niyonzima (Rwanda) na Ntibazonkiza (Burundi) ambaye katika mchezo wa juzi alifunga bao moja kwenye sare ya mabao 2-2 na kufikisha mabao manne kwenye michuano hiyo. 

Sehemu ya wachezaji wa Yanga ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu za taifa wanaendelea na mazoezi kwenye kambi yao ya Avic Town iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Mpaka sasa Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi, ambapo wamejikusanyia pointi 50 baada ya kucheza michezo 23.

Akizungumzia kuhusu mpango wa kuwarudisha nyota hao, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Haji Mfikirwa alisema: “Tayari tuliwapa mwongozo wachezaji wetu wote walioitwa kwenye vikosi vya timu ya Taifa kurejea mapema baada tu ya kumaliza majukumu yao ya kitaifa.

“Hivyo kwa kuwa wachezaji wetu wa kimataifa watakuwa na michezo Machi 29 na 30, basi tunaamini kuwa kuanzia tarehe 31 wataanza safari ya kurejea.

“Tunataka kuona kikosi kinakamilika mapema kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michezo yetu ijayo ya michuano ya Ligi Kuu Bara, na kombe la Shirikisho ambayo tuliweka wazi tunataka kushinda ubingwa,”

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic