March 28, 2021


 KLABU ya Manchester United inajiandaa kumuongezea mkataba mpya Ole Gunnar Solskjaer kuendelea kuwa kocha wa timu hiyo.

Imeelezwa kuwa mazungumzo ya mkataba huo mpya yataanza hivi karibuni licha ya kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwa bosi wa timu hiyo.


Kwa maana hiyo, Solskjaer anatarajiwa kupata nyongeza ya mshahara kutoka ule wa sasa anaolipwa pauni 7m (Sh bil 22.1) kwa mwaka.


United kwa sasa ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Premier League ikiwa nyuma ya wapinzani wao wa jiji moja, Manchester City ambao wana mwendelezo mzuri katika mbio za ubingwa wa Premier msimu huu.


Mkurugenzi Mtendaji wa United, Richard Arnold hivi karibuni alimsifia Solskjaer kwa kazi kubwa ambayo ameifanya.

 

Arnold alinukuliwa akisema:- “Unapokuwa ndani ya klabu na unaona maendeleo na mwenendo wake ulivyo anastahili kupata mafanikio hilo linanifurahisha," .


Tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo, Desemba 2018, Solskjaer hajafanikiwa kushinda taji lolote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic