March 27, 2021


 IMEELEZWA kuwa malalamiko ambayo Klabu ya Al Merrikh ya Sudan wameishtakia Simba yamekwama baada ya uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuwaambia kwamba waongeze ushahidi zaidi.

Al Merrikh wlipeleka malalamiko yao mbele ya Caf kwa kueleza kuwa walifanyiwa hujuma na mabosi wa Simba kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochewa Uwanja wa Mkapa.

Kupitia kocha wao mkuu, Lee Clark aliweka wazi kuwa kitendo ambacho walifanyiwa hakikuwa cha kiungwana jambo ambalo liliwafanya wapoteze mchezo wao huo muhimu.

Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu mazima ambazo zimewafanya waweze kuongoza kundi A wakiwa a pointi 10, huku Al Merrikh wakiwa na pointi moja ambayo waliipata kwa kulazimisha sare ya bila kufungana na Simba.

Malalamiko ya wapinzani hao wa Simba yalibainisha kuwa walihujumiwa kwa kigezo cha Corona ambapo wachezaji wao 8 waliambiwa kwamba wameathirikia na Corona ikiwa ni muda mfupi kabla ya mechi.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Al Merikh iliweka wazi kwamba wameonewa jambo ambalo wanaamini kwamba ilikuwa ni mbinu ya kuwashinda kiujanja.

Ikiwa malalamiko hayo yatakuwa na tija inaweza kupeekea Simba kupokwa pointi tatu na kupewa adhabu kutokana na sakata hilo jambo ambalo linawapa tabu Al Merikh kupambana ili kupata matokeo haraka.

6 COMMENTS:

  1. Kwani aliewapima na kuwakuta na corona ni Haji Manara hata wapokewe pointi tatu?

    ReplyDelete
  2. Utopolo ndio waliowapa akili ya kulalamika hawakujua kuwa Simba haihusiki na upimaji wa corona.

    ReplyDelete
  3. Huyu mwandishi nae sijui tumwite boy..? Unaletahii stori tena leo ya nini sasa. Achana na watu wasiojielwa. Ikiwa kwao wachezaji 5 walikutwa nayo, nini cha ajabu sasa

    ReplyDelete
  4. Nguruwe fc mbona mbona mnabwabwaja maneno

    ReplyDelete
  5. Utopolo fc kazi wanayo ,pili pili usiyo Ila yakuwashia nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic