March 10, 2021


 WAKIWA Uwanja wa Mkapa, mabingwa watetezi, Simba leo wamechezewa pira gwaride na kikosi cha Tanzania Prisons na kuwafanya wafanye msako mkali kutafuta bao la kufutia machozi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kipindi cha kwanza dakika ya 23, Chris Mugalu akiwa na kipa Jeremia Kisubi alipiga penalti iliyookolewa na kipa huyo wa Tanzania Prisons ambaye leo alikuwa kwenye ubora wake dakika zote 90 mpaka ubao ukasoma Simba 1-1 Tanzania Prisons.

Ni Salum Kimenya, kiraka wa Tanzania Prisons alianza kumtungua Aishi Manula dakika ya 56 kwa faulo aliyopiga nje kidogo ya 18 na ikapenya kwenye ukuta wa Simba na kumpoteza kipa namba moja Aishi Manula.

Baada ya bao hilo Didier Gomes alikuwa haamini anachokiona kwa kuwa vijana wa Prisons walikazana kucheza lile pira gwaride ambalo liliwafanya Simba wakazane kusaka ushindi huku mipango yao ikidhibitiwa.

Licha ya kwamba Prisons walikuwa 10 uwanjani baada ya Jumanne Elifadhil kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Mzamiru Yassin bado mambo yalikuwa mazito kwa Simba.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulikuwa unasoma Simba 0-1 Prisons jambo lililowafanya Prisons waamini watasepa na pointi tatu nyingine kama walivyowatungua bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela.

Katika dakika 5 za nyongeza zikiwa zinafika tamati, Luis Miquissone alimalizia pasi ya kichwa ya Bernar Morrison na kufanya ubao usome Simba 1-1 Prisons.

Sare hiyo inawafanya Simba wafikishe jumla ya pointi 46 wakiwa wamecheza mechi 20 huku wapinzani wao Yanga wakibaki kileleni na pointi zao 50 tofauti ya pointi 4.

Prisons wanafikisha jumla ya pointi 28 na wanapanda kutoka nafasi ya 10 mpaka ya 9.

19 COMMENTS:

  1. daaaa aiseee,,,penati,kadi nyekundu,dk 5 nyongeza,wachezaji 10,,,daaa Simba inabidi mumfanyie sherehe refa ni mwenzenu huyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba siyo Yanga , Simba ni timu kubwa inacheza dakika zote uwanjani siyo utopolo FC/Vidimbwi FC , Tusubirie hapo hapo kileleni ..Simba inakuja kuwaondoa maana hamjui maana ya Ubingwa

      Delete
  2. Naona leo waandishi mmefuraaahi hata kichwa cha habari kinaonesha hivyo.... Ila nawaona vilaza sana maana hamjui maana ya goli la kufutia machozi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba-yachezeshwa-pira-gwaride-muandishi bn hajui kama anakera watu

      Delete
  3. Refa alishindwa tu kushangilia lakini moyoni mwake alijawa na furaha tele baada ya goli kufungwa maana Simba walizitendea haki dakika tano zisizojulikana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmesahau prisons walivokuwa wakipoteza muda pasipo sababu yoyote!! Ngedere nyie

      Delete
    2. "VIMBURU" bila mipango ya refa mlikuwa mmeumia

      Delete
    3. Utopolo....Kama refa alikuwa upande wa Simba, basi angelikubali goli alolofunga Mugalu.

      Delete
  4. Kidimbwi FC kumbe bado Wana pumzi za ku comment Basi ngoja tuone baada Kama ya wiki kadhaa bakora zitalika pale Kidimbwi maana furaha yao ni Kama maisha ya mbu

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. Pira Birian wakiachiwa nafasi, wanaume wakikaza Pira kiporo, Kazi kujisifia tu.
    Haya sasa wachukue hizo point 3 za Prisons, wakachukungeza TFF kama kuna mchezaji alichezeshwa kimakosa, maana wao wakikosa point 3 uwanjani wanajaribu mezani, maana ilikua ktk hesabu za kuwafikia Yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesahau kesi zenu Kule cas jinsi ulivyojinga smb ilishatoka huko

      Delete
  7. kwa mtu makini sana tathimini ya benchi la ufundi inahusika.......kukosa mbinu namna ya kukabiliana na wachezaji pungufu uwanjani lkn pia timu yenye kila kitu

    ReplyDelete
  8. Prison wanacheza mpira qu vurugu tuu?

    ReplyDelete
  9. Utopolo so mtakutana na hao wahela jela kwenye FA? Jipigieni basi kama mnaweza pira buti

    ReplyDelete
  10. Kuna timu moja wiki iliyopita ilitoka sare mkoani ikalifukuza benchi lote la ufundi na hata hio timu ilikua pungufu lkn watu wameshasahau. Ama kweli kuna timu inahofia kivuli chake.... Mashabiki wake wameanza kuonekana tena mitandaoni na maneno ya kashfa, tunaombea watulie tuu, Simba na Yanga ni watani wa jadi ila sio matusi, wawe na subira tuu kama wameandikiwa ubingwa watapata ila si kwa matusi wapambane uwanjani na sio kwenye magazeti na mitandaoni...

    ReplyDelete
  11. Tantarira rira..paka mweusi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic