March 28, 2021




 WAKATI ubao ukisoma Netherlands 2-0 Latvia, kwenye mchezo wa kufuzu  Kombe la Dunia katika kundi G, Uwanja wa Amsterdam,  Mwanamama Stephanie Frappart alikuwa mwamuzi wa kati.

Ni Steven Berghuis dakika ya 32 na Luuk de Jong dakika ya 69 walimfanya Mwanamama huyo aweke mipira kati na kuwafanya Latvia wasiamini wanachokiona kwa kuyeyusha pointi tatu.

Ushindi huo unaifanya Netherlands kuwa nafasi ya 3 na pointi tatu  baada ya kucheza mechi tatu huku Latvia ikiwa nafasi ya 5 na imecheza mechi mbili haina pointi kibindoni. 

Stephanie ameweka rekodi ya kuwa mwamuzi wa kwanza kuchezesha mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia na pia amewahi kuweka rekodi ya kuwa mwamuzi wa kwanza Mwanamama kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa Desemba. 

Rekodi yake nyingine ilikuwa ni ya kuchezesha fainali ya UEFA Super Cup kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea 2019, Liverpool ilishinda kwa penalti.

Mwanamama huyo mwenye miaka 37 ni mpambanaji anastahili pongezi kwa kuandika rekodi nyingi nzuri kwenye ulimwengu wa mpira.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic