MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry ameachana na matumizi ya mitandao ya kijamii akishinikiza mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kutokomeza ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika.
Matukio ya ubaguzi yameshika kasi kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni hali inayowapa wasiwasi wachezaji wengi, huku kiungo ‘Fred’ wa Manchester United na Brazil akiwa mchezaji aliyekutana na matukio hayo siku tatu zilizopita.
Henry ambaye hivi karibuni aliacha kuiona klabu ya CF Montreal kutokana na sababu za kifamilia, alichapisha maneno makali kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’ akidai kujiondoa kwenye mitandao hiyo.
“Nitajiondoa kwenye mitandao ya kijamii mpaka pale watu wenye mamlaka husika watakapodhibiti vitendo hivi kwa nguvu na ukali ule ule ambao wanafanya wakati huu,” aliandika Henry.
0 COMMENTS:
Post a Comment