UKANDA wa Afrika Mashariki mambo yamekuwa magumu kwenye mechi za kuwania kukata tiketi ya kufuzu kushiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika, (Afcon) kwa timu nyingi kuangukia pua.
Sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 dhidi ya Cameroon inaifanya timu ya Taifa ya Rwanda nayo pia kuishia hatua ya makundi.
Ni Cameroon na Cape Verde wamekata tiketi ya kushiriki Afcon nchini Cameroon baada ya kuwa nafasi mbili za juu ambapo mwenyeji Cameroon ana pointi 11 huku Cape Verde akiwa na pointi 10.
Rwanda ipo nafasi ya 3 na pointi zao ni 6 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Msumbiji wenye pointi 4 baada ya kucheza jumla ya mechi 6.
Tanzania pia imeishia hatua ya makundi na pointi zake ni 7 katika kundi J ipo nafasi ya tatu ambapo ni Tunisia wenye pointi 16 na Equatorial Guinea wenye pointi 9 wamepenya mpaka Cameroon.
Burundi katika kundi E wapo nafasi ya tatu na pointi zao ni 5 huku Morocco yenye pointi 14 na Mauritania wenye pointi 9 wakitusua mpaka Cameroon.
Kenya katika kundi G ikiwa nafasi ya tatu na pointi zao ni 7 inafuatiwa na Togo yenye pointi 2, huku Misri yenye pointi 12 na Comoros yenye pointi 9 zikiibukia Cameroon.
Uganda katika kundi S wameishia nafasi ya 3 na pointi 8, Afrika Kusini ina pointi 3 nafasi ya nne, huku Burkina Faso yenye pointi 12 na Malawi yenye pointi 10 zimepenya .
Burundi nafasi ya tatu na pointi 5 katika kundi E na Afrika ya kati ipo nafasi ya nne na pointi 4, Morocco yenye pointi 14 na Mauritania yenye pointi 9 zimepenya.
Wamejitahidi wote wateleza kidogo
ReplyDelete