KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, raia wa Ufaransa amesema kuwa maandalizi ambayo wanayafanya kwa sasa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Congo yanakwenda vizuri na wana amini kwamba watapata matokeo chanya.
Simba inaendelea na mazoezi kwenye Viwanja vya Simba Mo Arena ambapo wanatarajiwa kucheza na AS Vita, Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.
Gomes amesema kuwa anahitaji kushinda kwenye mchezo huo ili kupata pointi tatu muhimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment