March 2, 2021


 LEO Machi 2, wachezaji wa kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco wanatarajiwa kuwasili ardhi ya Bongo wakitokea nchini Angola.

Wachezaji hao wawili ni Lukas Kikoti na Hamis Fakhi ambao walianza safari jana kwa kupitia Ethiopia wakitokea Angola walikokuwa wameshikiriwa karantini kwa zaidi ya siku 16.

Walikwama wakati walipkwenda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya 1 de Agosto pamoja na mwingine Fred Tangalo ambaye amebaki Angola.

Tangalo ambaye ni ingizo jipya kutoka ndani ya kikosi cha Lipuli amebaki Angola kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa majibu yake ya Corona bado hayajatoka.

 Namungo imetinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho na ipo kundi D.

4 COMMENTS:

  1. Hawa jamaa ni wajinga, hicho ni kitendo cha utekaji sasa. Serikali iingilie kati suala hili sio la kawaida

    ReplyDelete
  2. Ingekuwa ni mchezaji wa simba au yanga ingekuwa inshu kubwa kweli,,,naamini wangekuwa wameshaludi tz,,,kwakuwa inawahusu namungo naona wanaohangaika ni namungo peke yao,,,serikari imetulia tu lakini uwezo huo wanao sana wakuwasaidia,,,ngoja ije itokee kwa simba au yanga uone waziri wa michezo anavyohaha

    ReplyDelete
  3. Hii sasa inatia huruma sana, ni kama wametelekezwa. Sasa hata kama ana corona si wameache arudi huku kwetu corona is not a big deal atapona. Sasa muda wote huo waluomshikilia kama ni mgonjwa su atakuwa amekufa? Hui ni uhuni na unyanyasaji na udhalilishaji usiokubalika na dunia ya wastaarabu.

    ReplyDelete
  4. Tukipeleka lawama kwa serikali ni makosa. Tukumbuke ni serikali iliyo ingilia kati suala hili na ndio ikapelekea mechi zote zichezwe hapa bongo. Suala la watu wetu kuwekwa karantini huko ni utaratibu wa nchi ya Angola

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic