March 28, 2021


 ALLY Mayay, ‘Tembele’, kiungo wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kitu pekee ambacho kinaweza kuwapa matokeo chanya Simba kwenye mechi zake za kimataifa ni kuwa na nidhamu na kucheza kwa ushirikiano.

Aprili 3, Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya AS Vita ya Dr Congo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi.


Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Congo, Simba ilishinda kwa bao 1-0 ugenini na kusepa na pointi tatu jumlajumla.


Bao la ushindi lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Chris Mugalu ambaye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ametupia mabao mawili.


Akizungumza na Saleh Jembe, Mayay amesema kuwa itakuwa ngumu kwa Simba kupata matokeo chanya ikiwa watawadharau wapinzani wao na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo watazipata.


“Ukiwa nyumbani ni lazima ucheze kwa nidhamu na kutumia nafasi ambazo unazipata. Kwenye mashindano ya kimataifa nafasi moja ni muhimu kwa kuwa ukiikosa kurudi tena huwa inakuwa ngumu hivyo Simba lazima ijipange kwa ukamilifu.


“Imekuwa ikifanya vizuri kwenye mechi zake za kimataifa ila makosa ya safu ya ulinzi kutowasiliana uwanjani hilo ilikuwa kwenye mechi dhidi ya AS Vita pale walipokutana ugenini pamoja na kushindwa kutumia nafasi wanazotengeneza kama itaendelea kujirudia watakuja kujitia hapo baadaye,” amesema Mayay.


Kwenye kundi A, Simba ni namba moja wakiwa na pointi 10 kibindoni wanakutana na AS Vita ambayo ipo nafasi ya tatu na ina pointi 4 inahitaji kupata ushindi mbele ya Simba ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali.


Inakutana na Simba inayopambana kusaka pointi moja ili kutinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

1 COMMENTS:

  1. Huyo ni muungwana anayechululia mpira njia ya kujenga udugu na mapenzi na wala si uadui

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic