March 28, 2021


 KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Machi 28 ana kazi ya kukiongoza kikosi hicho kusaka ushindi mbele ya timu ya taifa ya Libya.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Kim kukiongoza kikosi hicho kwenye Uwanja wa Mkapa baada ya kurithi mikoba ya mtangulizi wake Etienne Ndayiragije. 

Mchezo wa leo ni maalumu kwa ajili ya kuwania kufuzu nafasi ya kuweza kushiriki Afcon nchini Cameroon ambayo tayari Stars imeshaikosa.

Taifa Stars mchezo wake uliopita ilikubali kufungwa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea, ulikuwa ni wa kwanza kwa Kim na ulipotwza matumaini ya Stars kuweza kufuzu Afcon.

Ipo kundi J ina pointi zake nne baada ya kucheza mechi tano. Inakutana na Libya ambayo ipo nafasi ya nne na ina pointi tatu baada ya kucheza mechi tano.

Hata Libya nayo imekwama kufuzu michuano hiyo mikubwa inayotarajiwa kuchezwa Cameroon.

Poulsen, Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao huo na wana amini watapata ushindi.

Kwenye kundi la Stars ni Equatorial Guinea yenye pointi tisa na Tunisia yenye pointi 13 wameweza kufuzu kushiriki Afcon nchini Cameroon.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic