IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta ipo tayari kumpa dili beki wa Inter Milan, Achraf Hakimi ambaye pia anapigiwa hesabu na Chelsea.
Kikosi cha Arsenal jana kililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Slavia Praha katika mchezo wa Europa League robo fainali ya kwanza jambo linaloongeza presha ya timu hiyo kutaka kufanya maboresho.
Ikiwa Uwanja wa Emirates, Arsenal ilishindwa kulinda bao lililopachikwa na Nicolas Pepe dakika 86 kwa kuruhusu wapinzani wao kuweka mzani sawa dakika ya 90+3 na Thomas Holes.
Kwa mujibu wa The Sun, Arsenal ipo kwenye hesabu za kumpata beki huyo ambaye ananolewa na Antonio Conte na amehusika katika mabao 12, amefunga sita na ametoa pasi sita kwenye mechi 36 msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment