DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezaji wake Bernard Morrison amekuwa akifanya majukumu yake kila anapopewa kwa kushirikiana na wengine.
Simba imetinga hatua ya robo fainali baada ya Aprili 3 kushinda mabao 4-1 dhidi ya AS Vita na Morrison alitoa pasi moja ya bao pia alionyeshwa kadi ya njano.
Leo Simba itakuwa na kibarua cha kumenyana na Al Ahly ikiwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba katika kundi A ikiwa ni mchezo wa 6.
Simba ina pointi 13 na Al Ahly ina pointi 8 zote zimefuzu hatua ya robo fainali kutoka kundi hilo na AS Vita yenye pointi 4 na Al Merrikh yenye pointi 2 hazijafuzu hatua ya robo fainali.
Gomes amesema:" Morrison amekuwa akitimiza majukumu yake na hii inatokea kwa wachezaji kutimiza majukumu yake jambo ambalo ni la msingi kama ilivyo kwake.
Kwani vipi, kuna anayeteseka?
ReplyDelete