April 17, 2021

 


USHINDI walioupata Azam FC jana mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara umewashusha Simba nafasi ya pili na kuwapeleka mpaka nafasi ya tatu.

Bao pekee la ushindi kwa Azam FC, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma lilipachikwa kimiani na Ayoub Lyanga dakika ya 21 na kuwafanya wenyeji, JKT Tanzania kukubali kuyeyusha pointi tatu mazima.

Azam inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imefikisha jumla ya pointi 50 baada ya kucheza mechi 26, Simba nafasi ya tatu imekaa baada ya kucheza jumla ya mechi 21 na imekusanya pointi 49.

Lyanga amesema kuwa ni furaha kuona timu inapata ushindi na watazidi kupambana kwa ajili ya mechi zao zijazo ndani ya ligi ili wafanye vizuri. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic