April 17, 2021


 JUMA Mwambusi Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa makosa ambayo waliyafanya kwenye mchezo dhidi ya KMC wameyafanyia kazi hivyo wataingia kwa kujiamini kusaka ushindi mbele ya Boashara United.

Mchezo wao uliopita Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Yanga 1-1 KMC na kuwadfanya kugawana pointi mojamoja. 

Leo Aprili 16 Yanga ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Biashara United mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara ubao ulisoma Biashara 0-1 Yanga hivyo leo utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Biashara United na Yanga itakuwa na kazi ya kulinda rekodi yake.

Mwambusi amesema:"Makosa ambayo tuliyafanya kwenye mchezo wetu uliopita tumeyafanyia kazi na tutaingia uwanjani kwa lengo la kupata pointi tatu.

"Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti, bado tuna mechi na ligi haijaisha chochote kinaweza kutokea," .


Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 51 na Biashara United ipo nafasi ya nne na pointi zake ni 40. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic