KOCHA mkuu mpya wa klabu ya Kagera Sugar, Francis Baraza
ametamba kuwa kikosi chake kitafanya vizuri katika michezo ijayo kutokana na
programu za mazoezi wanazoendelea kuzifanya.
Baraza alijiunga na Kagera Sugar na kutambulishwa rasmi Machi
17, mwaka huu akitokea kikosi cha klabu ya Biashara United ya mkoani Mara
aliyohudumu kwa misimu miwili.
Kocha huyo anatarajia kuiongoza Kagera Sugar kwa mara ya
kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Machi 8, mwaka huu.
Akizungumzia programu za mazoezi ya kikosi chake Baraza alisema: “Nashukuru kwa kupata nafasi ya kukiona kikosi changu na kufanya nao mazoezi kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa.
"Siwezi
kusema kuna mapungufu makubwa lakini tunafanya maboresho kidogo ya mbinu kwa
kuongezea kile walichokuwanacho na yale machache mapya ya kwangu,"
0 COMMENTS:
Post a Comment