April 17, 2021


 KLABU ya Bayern Munich inatarajiwa kuhusika katika kufanya mabadiliko makubwa klabuni hapo mara baada ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bayern iliondolewa katika Robo Fainali ya michuano hiyo na vigogo wa Ufaransa, Paris Saint-Germain, Jumanne ya wiki hii na hivyo kuvuliwa ubingwa.

 

Taarifa kutoka Ujerumani zinaeleza kuwa kunatarajiwa kufanyika mabadiliko makubwa kuanzia ndani hadi nje ya uwanja baada ya matokeo hayo.


Kwanza ni majaliwa ya kocha wao, Hansi Flick ambaye inaonyesha wazi kuwa hatakuwa klabuni hapo msimu ujao.


Kocha huyo amekuwa na msuguano na Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic, lakini pia kocha huyo anatajwa kuwa anaweza kuchukua mikoba ya Joachim Low katika timu ya taifa ya Ujerumani.

 

Mwishoni mwa msimu huu pia kutakuwa na wimbi kubwa la wachezaji wanaotarajiwa kuondoka wakiwemo Jerome Boateng, Javi Martinez na David Alaba.


Bayern inataka kuziba mapengo yao kwa kuwatumia Dayot Upamecano, Lucas Hernandez, Niklas Sule na Tanguy Nianzou.


Mkurugenzi Mtendaji Karl-Heinz Rummenigge ataondoka na nafasi yake itachukuliwa na kipa wa zamani wa timu hiyo, Oliver Kahn.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic