April 17, 2021


 MARWA Chamberi, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa na wanahitaji pointi tatu.

Biashara United inakumbuka kwamba mchezo uliopita dhidi ya Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 jambo ambalo litawafanya waingie uwanjani wakiwa na hasira za  kulipa kisasi.

Pia kwenye mchezo wao wa ligi uliopita wakiwa maskani yao pale Mara, Uwanja wa Karume walifungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union huku wapinzani wao Yanga wakiwa wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC, Uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo amesema:"Tunatambua kwamba tunakutana na Yanga ambayo ni timu kubwa tunaiheshimu ila haifanyi kwamba tuhofie kupata pointi tatu.

"Ukianzia kwa wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba haitakuwa kazi rahisi, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu," amesema.

Kwenye msimamo, Biashara United ipo nafasi ya nne na imekusanya jumla ya pointi 40 baada ya kucheza mechi 25 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 51 baada ya kucheza mechi 24.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa, majira ya saa 1:00 usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic