KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesifia klabu yake kwa kuweka historia mara baada ya Phil Foden kufunga bao la ushindi dhidi ya Borrusia Dortmund na kufanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza chini ya uongozi wake.
Foden alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo kumalizika usiku wa kuamkia jana.
“Kila mtu amefanya kazi kubwa klabuni, hii ni historia kubwa, nina furaha sana.”Man City sasa itakipiga dhidi ya PSG ya Ufaransa wakati Chelsea itaivaa Real Madrid katika nusu fainali
0 COMMENTS:
Post a Comment