BAADA ya kete yake ya kwanza akiwa kwenye benchi la ufundi Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi kushushudia ubao ukisoma Yanga 0-1 Azam FC amekabidhiwa dakika 630 za moto ambazo ni mechi 7 ndani ya Ligi Kuu Bara zenye alama 21.
Nabi raia wa Tunisia amekabidhiwa mikoba ya Cedric Kaze ambaye
alichimbishwa kazi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu ya
timu hiyo alianza mechi ya kwanza kwa kukaribishwa kwa kupoteza mbele ya Azam
FC.
Kigongo chako kijacho kwenye ligi ni Mei 8, itakuwa dhidi ya
Simba ambapo itakuwa ni dabi yake ya kwanza mchezo wao uliopita ubao
ulisoma Yanga 1-1 Simba.
Kisha Mei 15, itakuwa ni Namungo v Yanga walipokutana mzunguko
wa kwanza ubao ulisoma Yanga 1-1 Namungo. Mei 19 ana kazi ya kusaka ushindi
mbele ya JKT Tanzania walipokutana kwa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-0 JKT
Tanzania
Juni 19 ana kazi mbele ya Ruvu Shooting ambapo mzunguko wa
kwanza ubao ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting. Juni 22 atakuwa na Mwadui FC ambao
mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Mwadui 5-0 Simba. Julai 8, itakuwa mbele ya
Ihefu huku rekodi zikionyesha kwamba mchezo uliopita ubao ulisoma Ihefu 0-3
Yanga.
Nabi ikiwa bado atakuwa hajachimbishwa basi atakamilisha kete
yake ya mwisho ya dakika 630 mbele ya Dodoma Jiji, Julai 11, mchezo wa mzunguko
wa kwanza ubao ulisoma Yanga 3-1 Dodoma Jiji.







Lini Mwadui kaifunga Simba 5-0 ??
ReplyDeleteWaandishi wanashindwa kuyarejea tena waliyoyaandika na labda ilikuwa lengo ni kuyatamani hayo
ReplyDelete