JUMA Kaseja, nahodha wa kikosi cha KMC amesema kuwa wachezaji wote wa kikosi cha KMC ni bora jambo ambalo linampa nafasi kocha kuchagua aina ya wachezaji anaotaka waanze kikosi cha kwanza.
Mkongwe huyo kwenye eneo la milingoti mitatu aliwahi kucheza kwa
mafanikio ndani ya kikosi cha Smba ambapo huko pia alikuwa ni nahodha, pia
amecheza Yanga, Kagera Sugar na Mbeya City.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa jukumu la kocha
ni kujua aina gani ya wachezaji ambao anahitaji waanze kwa sababu wote wapo
vizuri na wanashirikiana.
"Tukipata matokeo tunafurahi na pale ambapo tunashindwa ni kazi ya kufanyia kazi makosa ambayo tunayafanya ila kikubwa ni kwamba tupo imara na tayari kwa ushindani na tunaendelea kupambana," amesema.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, KMC ipo nafasi ya 6 imekusanya pointi 36 baada ya kucheza mechi 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment