April 15, 2021

 


KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos, raia wa Angola mwenye mabao matatu na pasi mbili za mabao raia wa Angola adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata imekwisha kwa kuwa tayari mechi zake tatu ambazo ni dakika 270 zimekamilika.

Alionyeshwa kadi hiyo Februari 27, Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 baada ya kuonekana akimpiga ngumi beki wa Ken Gold, Boniphace Mwanjonde.

Alikosekana kwenye mechi tatu ilikuwa dhidi ya Coastal Union 2-1 Yanga , Uwanja wa Mkwakwani, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, na Yanga 1-1 KMC, Uwanja wa Mkapa.

Itakuwa ni jukumu la Kaimu Kocha wa Yanga, Juma Mwambusi kumpanga kwenye mchezo ujao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 17, ambao utakuwa ni wa ligi kati ya Yanga dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Kwenye msimamo Yanga iponafasi ya kwanza ina pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.


1 COMMENTS:

  1. Mmeanza tena na mitambo yenu ya mabao ambayo hayana madhara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic