MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anapenda kufunga muda mwingi akiwa uwanjani jambo linalomfanya aongeze juhudi.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Kagere ametupia jumla ya mabao 11 na timu yake imekusanya jumla ya pointi 49 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Namba moja ni watani zao wa jadi Yanga ambao wamekusanya pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.
Kagere amesema:"Ninapenda kufunga kwa kuwa mimi ni mshambuliaji na kila mshambuliaji anapenda kufanya hivyo kila akianza.
"Ushindani ni mkubwa nasi pia tunapambana ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu,".
Msimu uliopita Kagere alitupia mabao 22 na alisepa na kiatu cha ufungaji bora.
0 COMMENTS:
Post a Comment