April 16, 2021



KOCHA wa makipa wa Mtibwa Sugar, Soud

Slim amesema kuwa sababu kubwa ya timu

yake kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao 5-0

dhidi ya Simba, juzi Jumatano ni kwa kuwa

wachezaji wake wengi walikuwa katika mfungo

wa Ramadhan.

 

Mtibwa Sugar ilipata kichapo hicho katika

mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa

Mkapa jijini Dar.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Soud

alisema ilikuwa ni ngumu kwa timu yake

kukabiliana na ubora wa Simba wakiwa na

wachezaji wengi waliokuwa wamefunga jambo

ambalo lilisababisha wao kupoteza mchezo huo

kwa idadi kubwa ya mabao.

 

“Takribani wachezaji wetu nane walioanza

walikuwa kwenye swaumu, ilikuwa ngumu

kwetu kukabiliana na ubora wa Simba tukiwa

katika hali ile, nadhani hii ni moja ya sababu

iliyosababisha tukapoteza mchezo.

 

“Tunaamini huko mbeleni wachezaji watazoea

hii hali ya kucheza wakiwa wamefunga, kwani

ukiangalia ndiyo kwanza ilikuwa funga yao ya

kwanza lakini kwa jumla hatukuwa bora kabisa

uwanjani, tulifanya makosa mengi

yaliyosababisha kufungwa mabao mengi,

tunatakiwa kujiboresha zaidi,” alisema kocha

huyo.

 


1 COMMENTS:

  1. Sawa tumekusikia. Tulimsikia pia msemaji wenu, Kifaru, sasa nani anasema kweli?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic