April 9, 2021


 IMEFAHAMIKA kuwa Simba imetumia kitita cha shilingi bilioni moja katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Simba tayari imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika baada ya kuwafunga AS Vita mabao 4-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Aprili 3.

 

Timu hiyo imefuzu hatua hiyo ya makundi ikiwa inaongoza katika msimamo Kundi A, ikiwa na pointi 13 ikiwa imebakisha mchezo mmoja pekee dhidi ya Al Ahly utakaopigwa leo Ijumaa huko Cairo, Misri.


Taarifa zimeeleza kuwa Simba imetumia Sh 1Bil iliyotumika kwa ajili ya kuwapa bonasi wachezaji na benchi la ufundi.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa bonasi hiyo imetumika kwa ajili ya kuwaongezea morali na hali ya kujituma kwa wachezaji wake ili kufanikisha ushindi.

Aliongeza kuwa bonasi hiyo imehusisha michezo ya kimataifa pekee tofauti na Ligi Kuu Bara ambayo huko ipo bajeti nyingine inayojitegemea.

 

“Michuano ya kimataifa ina umuhimu wake, hivyo imetengwa bajeti maalum kwa ajili ya bonasi ya wachezaji wetu ambayo imetengwa katika makundi mawili.

 

“Makundi hayo kama timu ikifanikiwa ushindi kuna kiwango cha pesa ambacho wachezaji na benchi la ufundi, endapo timu ikipata ushindi na sare lakini timu ikifungwa hawapati bonasi.

 

“Hivyo hadi timu yetu inafanikiwa kufuzu robo fainali tumetumia kiwango cha Sh 1Bil kama sehemu ya bonasi kwa wachezaji na benchi la ufundi na hiyo ni katika kuwaongezea morali na hali ya kujituma,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mshauri wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Crescentius Magori hivi karibuni alizungumzia hilo la posho la wachezaji na kusema kuwa: “Hilo la posho lipo katika mikataba yetu kati ya wachezaji na uongozi.

 

“Hivyo wachezaji wetu tumewawekea utaratibu wa kuwapatia posho katika kuongeza morali ya ushindi pale wanapoipatia timu matokeo mazuri ya ushindi, hivyo hilo lipo katika timu yetu.”

3 COMMENTS:

  1. Hujui ulichokiandika,rudi darasani.

    ReplyDelete
  2. Sule za kata hizo ahsante kikwete, hatimae mnakuja kufanya upumbavu maeneo ya kazi alafu mkinyimwa ajira mnalalama, kumbe kichwani umebeba fb, Twitter, inst, YouTube, na wasap na ngono, ubongo wako bado ni old age hujawa renaissanced, try to rebirth brother.

    ReplyDelete
  3. Hii habari imejijenga kwenye roho mbaya na wivu zaidi kutokana mafanikio ambayo simba anaendelea kuyapata.Nadhani muandishi aende darasani kutafuta maana ya kuyeyusha hasa kwa maana ya matumizi ya pesa,kwa kifupi tu ni matumizi mabaya ya pesa. Sasa kwa mafanikio ya simba kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuitangaza kimataifa ni matumizi mabaya ya pesa basi tunawaandishi maamluki wasioitakia mema nchi yetu.Tukiacha utani wa simba na Yanga nikiri tu simba anafanya kitu kikubwa sana ambacho kwa taifa kwa sasa na ni wale watanzania wa kweli tu wenye akili timamu ndio wanaojua kazi wanayoifanya simba katika kipindi cha msiba wa taifa.Simba wanatufariji sana watanzania kutokana na machungu ya kuondokewa na kiongozi wetu mpendwa, mwanamaendeleo wa kweli hayati Magufuli. Simba walitufanya kukiona kipindi cha maombolezo kuwa kifupi. Hongereni simba nnaimani na simba na nadhani simba wakiwa makini kidogo kwenye hatua hii basi kombe la Africa hakuana wa kuwazuia kulitwaa huo ndio ukweli. Simba wawe Makini kivipi? Wasiridhike na kikosi chao cha sasa.Ni miongoni ya kikosi bora cha simba kuwahi kutokea kuanzia benchi la ufundi ila wanatakiwa kwenda kwenye robo finali na sapraizi kubwa zaidi itakatayowatkisa wapinzani wao. Sapraizi ipi hiyo? Wanatakiwa kuongeza sentafowadi mwengine matata. Sentafowadi mwenye sifa zote yakuwa sentafowadi.Simba wakifanikiwa kumpata fowadi mwenye sifa hiyo kuja kuongezea nguvu basi samba bingwa Africa kwa sababu backline ya simba ni chuma kiungo cha ulinzi ni chuma, fowadi ni chuma ila inahitaji extra sharpness au makali zaidi katika kugeuza nafasi za magoli kuwa magoli kwa ufasaha zaidi ni ngumu lakini wachezaji wa aina hiyo wapo wengi ingawa gharama ni lazima. Cha kuhofia labda kama mchezaji huyo ataweza kuendana na mfumo wa simba kwa uharaka ila anaejua anajua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic