KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema kwa mwendo wa mazoezi wanayofanya wachezaji wake, anaamini kwamba kwenye mechi za ushindani watakuwa na kazi ya kukimbiza wapinzani wao dakika zote 90.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23, mchezo wake unaofuata kwenye ligi ni dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Jumamosi hii.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mwambusi alisema mazoezi ambayo wanafanya vijana wake ni program maalum ambayo inaandaliwa kila siku na anamini inawajenga katika hali ya kujiamini.
“Kwenye mechi za ushindani ninaamini kwamba vijana watakimbiza dakika zote 90 kwa kucheza mpira bila kuchoka kwani mazoezi ambayo tunayafanya yanafuata kanuni zote za mchezo.
“Ikiwa vijana wanafanya mazoezi kwa muda wa zaidi ya dakika 90, ina maana kwamba watakuwa na uwezo wa kumudu muda kamili wa mechi, bado kuna mambo ya kuyafanyia kazi na tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” alisema Mwambusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment