KIKIWA kimejiwekea ngome nafasi ya 17 baada ya kucheza jumla ya mechi 25 na pointi zake 21 kikosi cha Ihefu FC leo kina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City.
Timu zote mbili maskani yao ni Mbeya na zinapambana kuweza kutafuta nafasi ya kubaki kwenye ligi kutokana na matokeo yao kuwa ya kususua msimu huu wa 2020/21.
Mbeya City wao wapo nafasi ya 16 baada ya kucheza jumla ya mechi 24 kibindoni wana pointi 21 hivyo leo atakayesepa na pointi tatu anaweza kujiondoa kwenye nafasi aliyopo kwa sasa.
Ihefu FC mchezo wake uliopita ilitoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Majaliwa.
Leo Aprili 15 ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Highland ambayo nayo pia ilitoka kugawana pointi mojamoja na Kagera Sugar, kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kocha wa Ihefu, Zuber Katwila amesema kuwa ushindani ni mkubwa na vijana wake amewaambia wajiamini ili wapate pointi tatu.
Hivyo leo wanaume 22 watakuwa kwenye vita ya Mbeya kupambana kujinasua kutoka nafasi za chini.
0 COMMENTS:
Post a Comment