April 15, 2021


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na nafasi waliyopo kwa sasa kwa sababu wanajua njia pekee itakayowafanya warejee nafasi ya kwanza na kuwashusha vinara wa ligi Yanga ni kushinda mechi zao.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 25 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya JKT Tanzania, Aprili 16.

Tayari kikosi kimeshawasili Dodoma na msafara wa wachezaji 25 pamoja na benchi nzima la ufundi kujiweka sawa na mchezo huo.

Vinara Yanga wana pointi 51 na wamecheza mechi 24 huku mabingwa watetezi Simba wakiwa wameweka utawala nafasi ya pili na pointi zao 49 baada ya kucheza mechi 21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Abdulkarim Amin, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa malengo yao yapo kwenye kushinda mechi zote ambazo watacheza.

“Mzunguko wa kwanza ulikuwa na ushindani mkubwa na tunaamini kwamba itakuwa hivyo kwenye mzunguko wa pili. Malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu jambo ambalo litatupa nafasi ya kuweza kuongoza ligi,” amesema Amin.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic