April 17, 2021


 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Klabu ya Arsenal, amesema kuwa nahodha wa kikosi hicho  Pierre-Emerick Aubameyang anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu kwa kuwa aliugua Malaria.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga bao katika ushindi wao wa mabao 3-0 wa Gabon dhidi ya DR Congo katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika, Machi 25, 2021.

 

Aliichezea Arsenal katika mchuano wao wa Kombe la Europa dhidi ya Slavia Praguetarehe Aprili 8, lakini alikosa mechi dhidi ya Sheffield United siku ya Jumapili ambapo Arsenal ilishinda.

 

“Nimekuwa hospitalini kwa siku chache wiki hii. Ninahisi nafuu kila siku kwa msaada wa madaktari bora waliogundua na kunitibu haraka….’ alisema kupitia Instagram Auba.


Arteta amesema:"Nimeongea naye anaendelea vizuri na yupo nyumbani. Maendeleo yake ni mazuri na alikuwa amelazwa siku mbili akipata matibabu hospitali na sasa anajiskia vizuri wamemruhusu," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic