April 6, 2021


 PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa anafikiria kusepa na tuzo ya mfungai bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 inayoshikiliwa na Meddie Kagere wa Simba.

Kagere alitwaa tuzo hiyo baada ya kutupia jumla ya mabao 22 na kwa sasa anaendelea kuisaka tuzo hiyo kwa kuwa ametupia mabao 9.

Dube ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina, ametupia jumla ya mabao nane na ametengeneza pasi tano za mabao.

Amekuwa kwenye mwendo mzuri katika kikosi hicho ambacho kwenye msimamo wa ligi kipo nafasi ya tatu na pointi zao ni 44.

Nyota huyo amesema:"Ninafurahi kuona kwamba timu inafanya vizuri na tunapata matokeo. Ninapenda kufunga kwa ajili ya timu na mafanikio yangu yapo nyuma ila ya timu yapo mbele.

"Hakuna mchezaji ambaye hapendi kupewa tuzo hata mimi pia ninatamani kuwa mfungaji bora hivyo nitapambana ili kuweza kufikia mafanikio,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic