April 6, 2021


UONGOZI wa Simba umesema kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuendelea kuwaombea dua wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ili waendelee kufanya vizuri kwa sababu ni faida kwa Tanzania kiujumla.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa msimu ujao Tanzania ikatoa timu nne kwenye mashindano ya kimataifa jambo ambalo ni la kujivunia na linasababishwa na wawakilishi wa Tanzania kwa wakati huu kwenye mashindano ya kimataifa.

Simba imetinga hatua ya robo fainali ikiwa kundi C na ina pointi 13 baada ya kucheza mechi tano mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili, 9 na leo kikosi kinatarajiwa kukwea pia.

Manara amesema:-"Watanzania watuombee kwa kuwa katika hili faida ni kubwa na kwa namna ambavyo tunakwenda sioni kama kuna nafasi kwa nchi nyingine kutuzidi kweye nafasi ya timu zitakaocheza kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

"Matumaini yetu ni kwamba kutakuwa na timu nne msimu ujao na hii imesababishwa na namba ya pointi ambazo Simba imeipata labda na Namungo pia.

"Simba inakwenda kutupa pointi ambazo mwakani Tanzania kutakuwa na timu nne ambapo mbili Kombe la Shirikisho na mbili Ligi ya Mabingwa,".


4 COMMENTS:

  1. Simba ipo kundi A sio C

    ReplyDelete
  2. Mechi ya Ahly kwa Simba isiwe mechi ya kujifurahisha bali iwe ni mechi ya maandalizi kwa ya mchezo wa robo final ugenini viongozi wa washikilie hapo. Zege hailali kazi kazi watanzania tuna Jambo letu mara hii.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic