KIKAO cha Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania, (Kamati ya Masaa 72) imetoa taarifa baada ya kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligu Daraja la Pili.
Katika taarifa iliyotolewa Aprili 16 maamuzi haya yamechukuliwa ambapo miongoni mwa timu zilizokutana na rungu hilo ni pamoja na Simba, Yanga, Azam FC, Dodoma Jiji:-
Mechi ya Coastal Union 2-1 Yanga, Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Kamati imezuia mashabiki wa timu zote kufika kwenye eneo la ushindani wa mchezo linalojumuisha eneo wanaloshukia wachezaji kutoka kwenye gari, eneo la vyumba vya kubadilishia nguo, eneo la kuchezea na eneo la benchi la ufundi.
Kagera 1-2 Azam FC, Klabu ya Azam FC imepewa onyo kali kwa kosa la wachezaji wa akiba na kocha wa viungo kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko.
Simba 1-1 Prisons, Simba imetozwa laki tano kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani wakati mchezaji wa Prisons alipokuwa akielekea vyumba vya kubadilishia nguo.
Polisi Tanzania 1-1 Yanga
Timu zote mbili zimepewa onyo kali kosa la mashabiki kuvuka uzio na kuingia uwanjani Machi 7,2021, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Dodoma Jini 0-0 Kagera Sugar, Klabu ya Dodoma imetozwa faini ya milioni moja kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina ambapo wakati wa mapumziko, Kagera ilikuta mlango wa chumba upo wazi, mayai yakiwa yamevunjwa mlangoni na ulikutwa udi uliochomwa.
Biashara United 1-1 Polisi Tanzania
Timu ya Polisi Tanzania imetozwa faini ya laki tano kwa kosa la shabiki wa timu hiyo kuwaga mtama getini wakati timu ya Polisi Tanzania ikiingia uwanjani tukio likiiashiria imani za kishirikina, Aprili 10, Uwanja wa Karume, Mara.
Shabiki wa Biashara United, Yohana Wilam amefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi 12 kwa kosa la kumtolea maneno ya kashafa na kumpiga kofi mchezaji wa Polisi Tanzania tukio lililosababisha ugomvi kati ya wachezaji wa Polisi Tanzania na Biashara United.
Mbeya City 0-0 Kagera Sugar
Timu ya Kagera Sugar imetozwa faini ya laki tano kwa kosa la kiongozi wao kuruka uzio wa ndani unaotenganisha mashabiki na wachezaji na kwenda chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji wa Kagera Sugar.
Ligi Daraja la Kwanza
Arusha FC 0-1 Geita
Kiongozi wa Arusha FC, ambaye ni Makamu Mwenyekiti Bwa. Emmanuel Minja amefungiwa kwa miezi sita kutojihusisha na mpira na faini ya laki tatu kwa kosa la kuvamia kikao cha maandalizi ya mchezo na kushinikiza kuwa timu ya Arusha FC isibadilishe jezi ya golikipa wakati jezi hiyo imefanana na jezi ya wachezaji wa ndani wa Geita Gold.
0 COMMENTS:
Post a Comment