April 16, 2021



MSHAMBULIAJI wa kikosi cha KMC, Charlse Ilanfaya amesema kuwa furaha yao kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Gwambina FC.

KMC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.

Ilanfya alitupia bao la ufunguzi dakika ya 51, Mvuyekure Emmanuel alitupia dakika ya 62 na msumari wa mwisho ulikuwa ni wa Oviedo, dk 72.


Ushindi huo unaifanya KMC kufikisha jumla ya pointi 39 na kupanda kutoka nafasi ya 6 mpaka ya tano baada ya kucheza mechi 26 huku Gwambina ikiwa na pointi 30 nafasi ya 10.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ilanfya amesema:"Furaha yetu ni kuona tunapata pointi tatu muhimu na kazi bado inaendelea," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic