April 16, 2021


 INAELEZWA kuwa aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amepeleka malalamiko yake ya madai ya stahiki zake kwenye Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA).

 Vandenbroeck ameipeleka Simba FIFA kudai malipo ya dola za Marekani 44,000 zaidi ya millioni 100 za kibongo, ambazo anadai ni malipo ya bonasi.


Inaripotiwa baada ya muda mrefu kuomba alipwe stahiki zake, mambo yalikuwa tofauti na alivyoahidiwa sasa amepeleka malalamiko yake FIFA.

Suala hili lilipelekwa FIFA wiki zilizopita na Shirikisho hilo la soka limethibitisha kuanza kulifanyia kazi shauri hilo.

Vandenbroeck alikiongoza kikosi cha Simba kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na alisepa baada ya kufanikisha malengo hayo ya Simba.

Kwa sasa kikosi hicho kipo mikononi mwa Didier Gomes ambaye amekifikisha kikosi hicho hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

5 COMMENTS:

  1. Ubinga mtupu, hadi aende Fifa tff ina taatifa kuhusu madai yake? Apambane na hali yake, haluna hela za ubwete huku. Aliyevunja mkataba ni nani. Kishingo akafie mbali huko na wapambe wake nuksi wanaomdanganya

    ReplyDelete
  2. Yaani uvunje mkataba tena kwa kusema uongo halafu unategemea Simba ni wapuuzi hivyo.

    ReplyDelete
  3. Kwahivo yeye ndie wa kumlipa Mnyama. Inawezekana kapata kiwewe juu ya mafanikio Makubw ya Mnyama ambayo alifikiri Simba baada ya kuondoka kwake itarejeya nyums

    ReplyDelete
  4. Kama alikatisha mkataba kwa hiari yake ni simba ndio wanaopaswa kulipwa. Ila ujinga kama huu wa taarifa kama hizi za kuipaka matope simba zinajitokeza tena kwa mara nyengine simba ikiielekea kupindua meza ligi kuu. Habari kama hivi zilijitokeza pia kipindi kile amabacho simba ilikuwa inakaribia kushika usukani wa ligi ndipo habari za timu ya Misri kuishtaki simba FIFA kwa Kichuya ambazo zilikuwa habari nu feki news. Ukitembelea mitandao ya kijamii hivi sasa utaona wameandika sijui uwanja wa Bunju wa Mo unataka kuuzwa kwa maseni,Sijui ujinga wa Billion Ishirini yaani baada ya simba kushindikana uwanjani sasa zinatumika kampeni chafu za nje ya uwanja kuitoa simba mchezoni. Naomba viongozi wa simba wanatakiwa kuwa wakali kidogo kuipigania Brand ya timu.
    Mitandao kibao inaandika habari za uongo halafu hakuna hatua zozote zinachukuliwa.Huko ni kuchafuliwa kwa klabu mjue Suala la kichuya lilikuwa feki kwa zaimira ya kuleta taharuki ndani ya simba lakini hatujajua mwisho wake ulikuwa vipi. Hao ni Matapeli mjue ni vyema mkawajulisha takukuru kwa kinga zaidi.

    ReplyDelete
  5. Kabisa wanaweweseka hawakutarajia we are another lever imeisha hiyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic