BAADA ya kutoonekana kwenye michezo ya
Ligi ya Mabingwa Afrika, wachezaji wa Simba
waliosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo, Junior
Lokosa raia wa Nigeria na Mzimbabwe Peter
Muduha, klabu hiyo imefunguka kuwa sababu
ya kuachana nao ni Kocha Mkuu, Didier Gomes
kutofurahishwa na viwango vyao.
Lokosa ambaye yeye ni mshambuliaji
alisajiliwa na Simba akitokea Esperance ya
Tunisia huku beki kisiki, Peter Muduha akitokea
Highlanders FC ya Zimbabwe.
Wachezaji hao walisajiliwa Januari, mwaka huu
kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambapo
mpaka sasa Simba imefuzu kuingia hatua ya
robo fainali huku wachezaji hao wakiwa
hawajacheza mchezo wowote.
“Wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni kwa ajili
ya kucheza michezo ya kimataifa ambao ni
Junior Lokosa na Peter Muduha watavunjiwa mikataba yao hivi karibuni.
“Wamekuwa na timu kwa muda mrefu lakini
bado viwango vyao havikuwa bora vya
kumridhisha Kocha Gomes, hivyo huenda
wakasitishiwa mikataba yao mwishoni mwa
msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Aidha, kwa upande wa Gomes wakati Simba
ikielekea Sudan kumenyana na Al Merrikh
alisema: “Wachezaji niliowaacha ambao
hawapo kwenye kikosi kinachosafiri akiwemo
Peter Muduha na Lokosa Junior sijafurahishwa
na viwango vyao.”
0 COMMENTS:
Post a Comment