April 16, 2021

 


RAIS wa Paris Saint Germain, (PSG), Nasser Al Khelaifi amesema kuwa  ana matumaini ya klabu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na anaamini kwamba nyota wake wawili, Neymar Jr na Kylian Mbappe watabaki kikosini hapo.

PSG imefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwaondoa mabingwa watetezi, Bayern Munich.



Rais huyo amesema:"Tumewekeza sana kuona kwamba tunafanikiwa na kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na makombe mengine.

"Kama tumewekeza sioni sababu ya Neymar na Mbappe kuondoka hapa kwa sababu tuna kila kitu na tunatakiwa kushinda kila kitu.

"UEFA bado haijamalizika ila tunatakiwa kupambana na msimu huu tuweze kufanya kitu cha tofauti," .

Mbappe alikuwa anatajwa kuibukia Real Madrid huku Jr yeye alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic